Advertisement · 728 × 90

Posts by JAHAZI la AKILI.

Teknolojia imetupa hisia kuwa kila kitu katika maisha kinaweza kufanikiwa haraka na kwa njia nyepesi kama taarifa tunazozipakua mitandaoni. Imepandikiza imani kuwa hatuna haja ya kutumia miaka kujifunza taaluma na stadi bali kupitia mbinu chache za udanganyifu.

1 week ago 0 0 0 0

Even our failures have a purpose.

1 week ago 0 0 0 0

"Wakati tunasheherekea sikukuu hii ya eid el fitr tuchukue nafasi hii kuwakumbuka ndugu zetu mashariki ya kati, Iran, palestina, Lebanon ambao siku hii imewafikia katika hali ya kukosa amani na kuondokewa na wapendwa wao. Mwenyezi Mungu azithibitishe nyoyo zao, awape subra na ushindi ulio karibu."

4 weeks ago 0 0 0 0

"Sikukuu ya Eid inaakisi furaha inayotawaliwa na kanuni na maadili ya kiislamu. Inaamrisha utu, upendo, heshima, tabasamu na kujali. Ni tukio la kutembeleana kwa ndugu, kupeana salamu, inafundisha huruma kwa wazazi na kuwajali wasiojiweza pamoja na majirani."
#Eidmubaraktoallbrotherandsister

1 month ago 0 0 0 0

"Kukaa na njaa kwa masaa 12 na kushiba kwa dakika 12 inaonyesha jinsi ambavyo starehe za maisha ya dunia zilivyo kuwa fupi na za kupita."

1 month ago 0 0 0 0
Post image

Great soul never dies.

1 month ago 0 0 0 0
Post image

Aliondoka khomeini akazaliwa khamenei. Kufa kwa Khamenei sio mwisho wa mapambano ni mwanzo wa hatua zingine mathubuti. Mwili unakufa ila fikra na falsafa zinazaliwa upya. Umeithibitishia dunia kuwa hukuwa muoga wala hukuhitaji kujificha kwa sababu ulikuwa unailinda haki.
#ShameonAmerican.

1 month ago 0 0 0 0

"Tunawatakia waislamu wote ulimwenguni mfungo mwema wa mwezi wa ramadhani. Mwenyezi Mungu atupe afya njema, atukubalie ibada zetu na atusamehe makosa yetu. tukaweze kuzibadili nafsi na roho zetu kutoka kanuni pekee za aridhini kuelekea maadili ya mbinguni."
#Ramadhanikareem.

2 months ago 0 0 0 0

Kufika kwa mwezi wa msamaha.
"Anasimulia Abuu Huraira (r.a) kuwa amesema Mtume (s.a.w) ibada ya swala tano, na kutoka ijumaa moja hadi nyingine, na kutoka ramadhani moja hadi nyingine ni sababu ya kufutiwa madhambi yaliyotendwa kati ya nyakati hizo pale ambapo madhambi makubwa yameepukwa."

2 months ago 0 0 0 0

"Duniani hakuna uwezekano wa kuishi milele lakini kuna uwezekano wa kufanya ukumbukwe milele. Uwepo wetu tuufanye uwe sababu ya faraja kwa wengine. Afya, akili, elimu, mali na muda vyote hivi vinaweza kutufanya tukumbukwe milele endapo vitatumika katika njia sahihi."

2 months ago 0 0 0 0
Advertisement

"انا للله وانا اليه راجعون.
#We are all belongs to Allah and to Him is our return."

2 months ago 0 0 0 0

"Maisha yetu yana namna ya kujirudia. Ni kama sauti ya mwangwi unayoitoa kisha inajirudia. Lolote zuri au baya unalolifanya kwa mwingine lazima kuna siku litakurudia tu. Hata kama sio wewe atakuwa mwanao, hata kama sio mwanao basi atakuwa mjukuu wako. Tuwe wazuri ili wanaokuja pia wawe wazuri."

2 months ago 0 0 0 0

"Binadamu ameweza kuogelea baharini kama samaki, ameweza kupaa angani kama ndege, lakini ameshindwa kutembea nchi kavu kwa uadilifu. Kadri teknolojia inavyozidi kukua ndivyo binadamu anavyozidi kupoteza utu wake"

2 months ago 0 0 0 0

Wakati ulimwengu ukiwa kimya, Qur'an inakuwa ni ulimwengu unaosema na kuzungumza, inamtaka mwanadamu kufungua akili yake na fikra zake kwa mapana. kwa kuyahifadhi na kuyaelewa maudhui yake dunia inabaki salama, na wanadamu wanapata utukufu duniani na Akhera. #Qur'anmybook.

2 months ago 0 0 0 0
Post image
2 months ago 0 0 0 0
Post image

"You reap what you sow. Misfortune are your choice. By blaming you lose your power, and by complaining you scatter happiness." #theartoflife.

2 months ago 0 0 0 0

"Na tazama baada ya mda wote huu, JUA halijawahi kuiambia DUNIA umenichosha!!. Angalia ni upendo wa namna gani huo, bado hueneza mwanga wake kote angani. Hadithi za mafanikio yetu zitasimuliwa kwa alfabeti za kuwahudumia wengine"

2 months ago 0 0 0 0

"Tupo katika zama ambazo ndoa siyo tena jambo la heshima kwa mwanamke bali uwanja wa mapambano kati ya mwanaume na mwanamke. Ushindani huo unazidi kuenezwa, jambo pekee litakalo ondoa hali hii ni wao kurudi na kuishi kwa misingi ya Qur'an na sunna." #Kutokandoahadipeponi.

2 months ago 0 0 0 0
Advertisement
Post image

Back to school. 2017 kwadelo sec. School.

2 months ago 0 0 0 0

"Kuna utajiri mkubwa kuliko afya? Kuna furaha kubwa kuliko amani? Kuna neema kubwa kuliko uislamu? Kuna utukufu zaidi ya uchamungu?
Dunia hukosa thamani kwa mtu aliyeshindwa kupata haja ndogo. Kwa kukosa hekima na siri za baadhi ya mambo tunalalamika kwa vitu tulivyopaswa kushukuru"

2 months ago 0 0 0 0
Post image

"Be a human or try to save humanity. Because of humanity our planet seem to be a safe place to live, otherwise there's no meaning of life." #free #palestine.

2 months ago 0 0 0 0

"Moyo si wa kila mpitaji, ni amana. Na mapenzi bila taqwa ni safari ndefu isiyo na dira. Ewe nafsi yangu usinigeuke nikihitaji onyo, nikumbushe nikighafilika. Nahitaji mkweli pembeni yangu, nimechoka majaribu."

2 months ago 0 0 0 0

"Katika hali yoyote ambayo Mwenyezi Mungu anatunyanyua sio tu ni kwa ajili yetu bali pia kwa ajili ya wengine. Tunapopitia njia ngumu ni ili tujenge kumbukumbu kuwa hayo ndiyo maisha ya wengine ya kila siku. Kwa kuwaangalia walioko chini yetu ndipo tunapoyapa maisha maana kamili."

2 months ago 0 0 0 0
Post image

I think paradise will look like library.

2 months ago 0 0 0 0

"Mwanamke anazidi kuwa mzuri zaidi kwa tabia njema, nafsi yenye kushukuru, moyo wenye kuridhika na jicho lisilo na tamaa. Kwa akili yake kubwa anakuwa amebeba dhima ya mwanamke halisi na nguzo tegemeo ya ulimwengu"

2 months ago 0 0 0 0

"Ni asili ya mwanadamu kukata tamaa hasa pale anapokosa faraja na kutiwa moyo. Tunapokosa faraja kutoka kwa wengine tuna kimoja kilicho ndani yetu nayo ni IMANI kamwe tusiipoteze."

2 months ago 0 0 0 0

"Miaka 100 ijayo dunia haitajali nilikuwa nani, niliishi wapi na niliishi maisha ya namna gani isipokuwa dunia itakuwa tofauti kwa sababu nilikuwa makini katika malezi ya mtoto."

2 months ago 0 0 0 0
Advertisement

"Kila jambo huanzia kwenye ugumu kwenda kwenye wepesi. Bahati mbaya zaidi huwa hatujui ni sehemu gani huwa tumebakisha kufika katika kelele cha mafanikio pale tunapoanza kukata tamaa. Mafanikio makubwa hupatikana pindi subira inapovuka kiunzi cha majaribu"

2 months ago 0 0 0 0
Post image

"Na wale wanaosema Mola wetu Mlezi tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamungu." 25:65

2 months ago 0 0 0 0

"Ibada ya sala inatufundisha unyenyekevu na utii wa kiwango cha juu kwa Muumba wetu. Kuliweka chini paji la uso ambayo ni sehemu ya thamani na anayojivunia mwanadamu ni ishara ya kuwa pamoja na vyote anavyovimiliki mwanadamu bado ni dhalili mbele ya Mola wake."

2 months ago 0 0 0 0